Simba yaifuata Singida Black Stars

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th March 2026


Simba yaifuata Singida Black Stars

Kikosi cha Simba kimeondoka jijini Dar es salaam leo Jumatatu, March 09 kuelekea Singida tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars.

Mchezo huo wa kwanza kuzikutanisha timu hizo msimu huu, utapiigwa Jumatano, March 11 katika uwanja wa Airtel, Mtipa.

Simba inatarajiwa kuweka kambi ya siku moja mkoani Dodoma kabla ya kuelekea Singida mapema Jumanne.

Mtanange huo unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini kwani mechi baina ya timu hizo hazijawahi kuwa nyepesi.

Singida BS watakuwa na shauku ya kujisahihisha baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa mabao 3-0 na Yanga wakati Simba imetoka sare mbili mfululizo mechi za ligi dhidi ya Dodoma Jiji na Yanga.

Singida BS imetangaza viingilio vya mchezo huo


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.