International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu March 09 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Mar 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu March 09 2026

Callum Wilson akubali kusalia West Ham, Ibrahim Sangare aongezwa kwenye orodha ya wanaowindwa na Manchester United na Manchester City yakaribia kumsajili Tino Livramento. Mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 34, amekubali mkataba mpya wa mwaka mmoja na West Ham wiki chache tu baada ya kuonekana kuwa mwenye kuondoka hivi karibu. (Telegraph - subscription required)

Manchester United imemuongeza kiungo wa Nottingham Forest wa Ivory Coast Ibrahim Sangare, 28, kwenye orodha ya wachezaji inaowataka wajiunge nao msimu huu wa joto. (CaughtOffside)

Manchester City inakaribia kumsajili beki wa pembeni wa Newcastle United, Tino Livramento, 23. (Football Insider) Newcastle waonyesha nia thabiti ya kumsajili kiungo mahiri wa Uingereza Marcus Tavernier, 26, kutoka Bournemouth. (Teamtalk).

Wachunguzi wa Real Madrid walimtazama kiungo wa kati wa Italia Sandro Tonali, 25, akiwa uwanjani, wakati timu yake ya Newcastle ilipotolewa kwenye Kombe la FA na Manchester City siku ya Jumamosi. (Sun).

Andy Robertson wa Liverpool anasema mazungumzo kuhusu mustakabali wake hayatatangazwa hadharani baada ya beki huyo wa kushoto wa Scotland, 31, kukaribia kujiunga na Tottenham mnamo mwezi Januari. (Athletic - subscription required).

Arsenal wako kifua mbele katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Leon Goretzka, mwenye umri wa miaka 31. (Christian Falk)

Winga wa Ujerumani Julian Brandt, 29, ataondoka Borussia Dortmund kwa uhamisho wa bila malipo mwishoni mwa msimu. (Sky Sports)

RB Leipzig wamekubaliana kuhusu masharti binafsi na kiungo mkabaji wa Borussia Monchengladbach Rocco Reitz, huku vilabu hivyo viwili vikiwa katika mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23. (Florian Plettenberg)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
6h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’