Local,Normal News,Simba, Mamelodi

Rushine afichua siri ya kuongeza mkataba Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Mar 2026
Rushine afichua siri ya kuongeza mkataba Simba

Beki wa Simba Rushine de Reuck amesema mapokezi mazuri na sapoti anayopata kutoka kwa Wanasimba ni moja ya sababu iliyopelekea akubali kuendelea kuitumikia Simba kwa muda mrefu zaidi.

Rushine jana alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Simba ambao utamfanya asalie Msimbazi hadi mwishoni mwa msimu wa 2027.

"Nimefurahi sana kuongeza mkataba kuendelea kusalia hapa. Tangu siku nilipojiunga na Simba, nimekuwa na uhusiano wa kipekee na mashabiki wa Simba."

"Wamenipokea vizuri na pia wananipa ushirikiano hivyo uamuzi huu wa kuongeza mkataba ni kama kurudisha shukrani kwao," alisema Rushine.

Rushine ambaye amekabidhiwa majukumu ya unahodha msaidizi wa Simba, amekuwa na wakati mzuri tangu alipojiunga na Simba kwenye usajili uliopita wa dirisha kubwa akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Wakati anatua alisaini mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja ambao ulikuwa na kipengele cha kuongeza mwaka wa pili.

Beki huyo alikuwa akiwaniwa kwa karibuni na Raja CA inayonolewa na kocha Fadlu Davids ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa kumleta Simba wakati anawanoa Wekundu hao wa Msimbazi.

Simba pia imemuongeza mkataba kiungo wake mkabaji Yusuph Kagoma ambaye ameongeza mkataba wa miaka miwili ambao utamuweka Msimbazi hadi mwaka 2028.

>>> XTRA 90 MEDIA imetangaza nafasi za kazi. BONYEZA HAPA

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’