Tanzania Prisons vs Yanga kupigwa Tabora

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th March 2026


Tanzania Prisons vs Yanga kupigwa Tabora

Tanzania Prisons imethibitisha yake dhidi ya Yanga itapigwa mkoani Tabora kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Ni baada ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kutangaza kufungia uwanja wa Sokoine jana Machi 8, 2026.

Mtendaji Mkuu wa Tanzania Prisons, Ajabu Kifukwe, amesema tayari wameandika barua TFF juu ya uamuzi wao wa kutumia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wa mkoani Tabora wakati uwanja wa Sokoine ukiendelea na ukarabati.

"Mchezo wetu dhidi ya Yanga utachezwa Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, tumejipanga kushinda baada ya kutokuwa na mwanzo mzuri, ari ya wachezaji iko juu na tunawaomba radhi mashabiki wetu kwa mabadiliko haya yaliyo nje ya uwezo wetu," alisema Kifukwe

Tanzania Prisons na Yanga zitaumana siku ya Alhamisi, March 12 ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya NBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.