Michuano ya ligi ya Muungano 2026 inatarajiwa kuanza visiwani Zanzibar April 21 ikitarajiwa kushirikisha timu nane ambapo nne zitatoka Zanzibar na nne zikitoka Tanzania Bara.
Timu za Yanga, Simba, Azam Fc na Singida Black Stars zinatarajiwa kushiriki zikitokea Tanzania Bara huku Mlandege FC, Muembe Makumbi City, Mafunzo na KVZ zikitokea Zanzibar.
Β Yanga ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Muungano baada ya kulibeba mwaka jana 2025 kwa kuifunga JKU bao 1-0 katika fainali iliyochezwa Mei Mosi, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Kwa kutwaa ubingwa huo, iliifanya Yanga kuwa kinara baada ya kulibeba mara saba ikifanya hivyo mwaka 1983, 1987, 1991, 1996, 1997, 2000 na 2025.
Michuano hiyo itachezwa kwa siku tano ambapo itafika tamati April 26 siku ya kilele cha Muungano.