Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Singida

Kombe la Muungano kutimua vumbi April 21

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Mar 2026
Kombe la Muungano kutimua vumbi April 21

Michuano ya ligi ya Muungano 2026 inatarajiwa kuanza visiwani Zanzibar April 21 ikitarajiwa kushirikisha timu nane ambapo nne zitatoka Zanzibar na nne zikitoka Tanzania Bara.

Timu za Yanga, Simba, Azam Fc na Singida Black Stars zinatarajiwa kushiriki zikitokea Tanzania Bara huku Mlandege FC, Muembe Makumbi City, Mafunzo na KVZ zikitokea Zanzibar.

Β Yanga ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Muungano baada ya kulibeba mwaka jana 2025 kwa kuifunga JKU bao 1-0 katika fainali iliyochezwa Mei Mosi, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.

Kwa kutwaa ubingwa huo, iliifanya Yanga kuwa kinara baada ya kulibeba mara saba ikifanya hivyo mwaka 1983, 1987, 1991, 1996, 1997, 2000 na 2025.

Michuano hiyo itachezwa kwa siku tano ambapo itafika tamati April 26 siku ya kilele cha Muungano.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’