International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne March 10 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Mar 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne March 10 2026

Juventus wana nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Tottenham na Uingereza Djed Spence, 25, msimu huu wa joto (Gazzetta dello Sport - in Italian).

Liverpool wanafikiria kumsajili winga wa Al-Ittihad na Ufaransa Moussa Diaby, mwenye umri wa miaka 26, huku mchezaji huyo wa zamani wa Aston Villa akitaka kuondoka katika klabu hiyo ya Saudi Pro League msimu huu wa joto. (Teamtalk).

Newcastle wameazimia kumshikilia kiungo wa kati Bruno Guimaraes, 28, na wanafanya mazungumzo ya mkataba na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Caughtoffside).

Real Madrid yamweka kocha mkuu wa Marekani na kocha wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino, kwenye orodha ya watakaowania kuchukua fursa ya Alvaro Arbeloa huko Bernabeu kabla ya msimu ujao. (ESPN).

Manchester United haitakimbilia kumteua kocha wa kudumu licha ya kocha wa muda Michael Carrick kuwasilisha matakwa yake. (The Athletic - usajili unahitajika).

Beki wa Newcastle na Uingereza Tino Livramento, 23, hayuko karibu kukubali kujiunga na Manchester City katika mkataba wa majira ya joto licha ya uvumi. (Fabrizio Romano).

Kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 27, hana mpango wa kufanya mazungumzo na Liverpool kuhusu mkataba mpya msimu huu wa joto lakini anafurahia kuwa Anfield licha ya kuhusishwa na Real Madrid. (Mundo Deportivo - in Spanish).

Mshambuliaji wa West Ham Callum Wilson amekubaliana kwa maneno kuhusu mkataba mpya wa mwaka mmoja licha ya Celtic kuvutiwa na Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 34. (Sky Sports).

Manchester City huenda wasiondoe kipengee ambacho kitamfanya kiungo mahiri wa Marekani mwenye umri wa miaka 16, Cavan Sullivan, ajiunge nao kutoka klabu ya MLS Philadelphia Union msimu ujao. (The I - subscription required).

Kuna kipengele katika makubaliano ya awali ambacho kiliruhusu City kumtoa katika klabu ya MLS mapema ikiwa angeonyesha kuwa na matokeo mazuri kwa haraka lakini kuna uwezekano mdogo hilo litafamyika.

Kiungo wa zamani wa Tottenham Ryan Mason ndiye mgombea anayeongoza kuchukua nafasi ya Igor Tudor kama kocha wa muda wa Spurs. (Football Insider).

Bayer Leverkusen itazingatia mustakabali wa kocha Kasper Hjulmand mwishoni mwa msimu. (Florian Plettenberg).

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’