Inaelezwa mabosi wa Simba wameanza mapema mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Asec Mimosas, Souleymane Fofana, imefahamika.
Fofana amekuwa na kiwango bora msimu huu akiifungia Asec jumla ya mabao 11 na asisti 5 katika mechi 17 tu.
Simba inamtaka mshambuliaji huyo ambaye pia anaweza kutumika kama namba 10 achukue nafasi ya Jonathan Sowah ambaye uwezekano wa kuendelea kusalia Msimbazi ni mdogo.
Asec inafahamika kwa kutoa wachezaji wenye vipaji ambao baadhi yao wamecheza hapa Tanzania wakiwemo Aubin Kramo na Zana Koulibay ambao wamewahi kuitumikia Simba.
Rais wa timu hiyo Roger Ouegnin ameweka wazi kuwa watakuwa tayari kufanya biashara na Simba au timu nyingine yoyote itakayomuhitaji mshambuliaji ambaye msimu huu amekuwa gumzo.
βHadi sasa hatujapokea ofa yoyote kutoka Simba, Fofana ni mchezaji wetu anaendelea kutumikia mkataba wake, wote tunafurahia kiwango chake,β Ouegnin alinukuliwa na Mwanaspoti.
βASEC hatuna shida kwenye kufanya biashara kwa wachezaji, kama tukikubaliana kila kitu kinawezekana lakini huyu Fofana ana ofa nyingi sana hapa Afrika na hata Ulaya, kwetu sisi tutaangalia kipi kitafikia mahitaji tunayoyataka na tunaweza kumuachia mchezaji."