Local,Transfer News,Simba, Asec

Simba yampigia hesabu mshambuliaji Asec

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Mar 2026
Simba yampigia hesabu mshambuliaji Asec

Inaelezwa mabosi wa Simba wameanza mapema mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Asec Mimosas, Souleymane Fofana, imefahamika.

Fofana amekuwa na kiwango bora msimu huu akiifungia Asec jumla ya mabao 11 na asisti 5 katika mechi 17 tu.

Simba inamtaka mshambuliaji huyo ambaye pia anaweza kutumika kama namba 10 achukue nafasi ya Jonathan Sowah ambaye uwezekano wa kuendelea kusalia Msimbazi ni mdogo.

Asec inafahamika kwa kutoa wachezaji wenye vipaji ambao baadhi yao wamecheza hapa Tanzania wakiwemo Aubin Kramo na Zana Koulibay ambao wamewahi kuitumikia Simba.

Rais wa timu hiyo Roger Ouegnin ameweka wazi kuwa watakuwa tayari kufanya biashara na Simba au timu nyingine yoyote itakayomuhitaji mshambuliaji ambaye msimu huu amekuwa gumzo.

β€œHadi sasa hatujapokea ofa yoyote kutoka Simba, Fofana ni mchezaji wetu anaendelea kutumikia mkataba wake, wote tunafurahia kiwango chake,” Ouegnin alinukuliwa na Mwanaspoti.

β€œASEC hatuna shida kwenye kufanya biashara kwa wachezaji, kama tukikubaliana kila kitu kinawezekana lakini huyu Fofana ana ofa nyingi sana hapa Afrika na hata Ulaya, kwetu sisi tutaangalia kipi kitafikia mahitaji tunayoyataka na tunaweza kumuachia mchezaji."

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’