Local,Normal News,Simba, Singida

Makocha Simba, Singida BS watambiana

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Mar 2026
Makocha Simba, Singida BS watambiana

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema kikosi chake kimejiandaa kushinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Airtel huko Singida.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Barker alisema hawakushinda mechi mbili zilizopita kwenye ligi hiyo mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwao kushinda.

"Ni mchezo muhimu sana kwetu, hatukushinda michezo miwili liyopita, hivyo huu ni mchezo muhimu kwetu kushinda ili kurejea kwenye nafasi nzuri katika mbio za ubingwa."

"Tunatambua Singida BS ni timu nzuri wamekuwa na msimu bora mpaka sasa pia wana kocha mzuri hivyo lazima tuhakikishe kesho tunacheza katika ubora wetu ili tuwe na nafasi nzuri ya kushinda."

"Tunawaahidi mashabiki wetu tutajiandaa vyema na kucheza katika mpango sahihi wa mchezo ili tuhakikishe tunawapa furaha," alisema Barker

Nae kocha msaidizi wa Singida Black Stars David Ouma, amesema wamejiandaa kutumia vyema uwanja wa nyumbani na kuondoka na ushindi katika mchezo huo.

Ouma amesema malengo ya Singida BS msimu huu ni kutwaa ubingwa hivyo wanapaswa kushinda mechi kubwa ili kufikia matarajio yao.

"Sisi Singida tunajiona kama moja ya timu zinazowania ubingwa wa ligi kuu. Ili uwe bingwa unapaswa kushinda mechi kubwa kama hii dhidi ya Simba. Hivyo tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi," alisema Ouma

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’