Tanzania Prisons vs Yanga ni Dodoma

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th March 2026


Tanzania Prisons vs Yanga ni Dodoma

Klabu ya Yanga imethibitisha kupokea taarifa rasmi kutoka kwa Bodi ya ligi kuwa mchezo wake dhidi ya Tanzania Prisons utapigwa Alhamisi, March 12 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Kumekuwa na mkanganyika juu ya wapi mchezo huo utapigwa jana Tanzania Prisons ikitangaza kuchagua uwanja wa Ali Hassan Mwinyi huku kikosi cha timu hiyo kikiwasili Tabora mapema leo.

Hata hvyo taarifa rasmi ni kuwa mchezo huo sasa utapigwa Dodoma, hivyo Prisons watalazimika kusafiri kutoka Tabora kuelekea Dodoma.

Klabu ya Yanga ilikuwa bado haijasafiri ikisubiri taarifa rasmii ya Bodi na sasa mabingwa hao watetezi wametangaza kuelekea mkoani Dodoma hapo kesho.

Awali mchezo huo ulipangwa kupigwa uwanja wa Sokoine lakini uwanja huo umefungiwa na TFF baada ya kukosa vigezo vya kikanuni.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.