Dodoma Jiji 'wametepeta' uwanja wa nyumbani, Jamhuri mkoani Dodoma wakikubali kipigo cha mabaoo 3-0 kutoka kwa Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Zidane Seleli alikuwa shujaa wa Azam Fc katika mchezo huo akifunga mabao mawili dhidi ya waajiri wake wa zamani huku Feisal Salum 'Fei Toto' akirejea na bao na asisti baada ya kumaliza adhabu ya kukosa mechi mbili kufuatia kadi nyekundu aliyopata katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji.
Baada ya kukosa ushindi katika mechi mbili zilizopita, hatimaye Azam Fc imerejea katika mwendo wa kukusanya alama tatu, ushindi huo ukiwasogeza hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo kwa tofauti ya mabao baada ya kufikisha alama 27 sawa na Simba liyopata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida BS katika mchezo wa mapema.

Mchezo unaofuata kwa Azam Fc ni dhidi ya Yanga, utakaopigwa March 15 katika uwanja wa Benjamini Mkapa, dabi ya Dar es salaam.