Local,Normal News,Simba, TRA

Mkataba wambana beki TRA United kucheza dhidi ya Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Mar 2026
Mkataba wambana beki TRA United kucheza dhidi ya Simba

Timu ya TRA United iliyohamishia makazi yake mkoani Arusha, kesho Jumamosi March 14 itakuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Katika mchezo huo TRA United watamkosa beki wao tegemeo Chamou Karabou ambaye anatumikia timu hiyo kwa mkopo akitokea klabu ya Simba.

Makubaliano ya kimkataba baina ya TRA United na Simba, yanamzuia Chamou kucheza dhidi ya waajiri wake hao, klabu ya Simba.

Chamou amekuwa na kiwango kizuri tangu ajiunge na TRA United akiwa ameifungia timu hiyo moja ya mabao kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo uliopita.

Hata hivyo TRA United wanaweza kumtumia kiungo 'punda' Mzamiru Yassin ambaye nae alijiunga na timu hiyo kwa mkopo kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Simba.

Valentine Nouma ni mchezaji mwingine ambaye pia anaitumikia TRA United akiwa nae amewahi kupita kunako klabu ya Simba.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’