International,Normal News,Berkane, Hilal, Local

Berkane chupuchupu nyumbani mbele ya Al Hilal katika Robo Fainali CAF Champions League

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Mar 2026
Berkane chupuchupu nyumbani mbele ya Al Hilal katika Robo Fainali CAF Champions League

Klabu ya RS Berkane ya Morocco imelazimishwa sare ya 1–1 na Al Hilal Omdurman ya Sudan katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya mashindano ya CAF Champions League uliochezwa Jumamosi, Machi 14, 2026 kwenye Uwanja wa Municipal mjini Berkane.

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa huku kila timu ikijaribu kupata faida kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Sudan.

Wageni Al Hilal ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza mapema katika mchezo huo baada ya mshambuliaji Abu Aqla Omer kufunga dakika ya 13, akimalizia vizuri pasi ya Abdelraouf Yagoub na kuwapa timu yake matumaini ya ushindi ugenini.

Baada ya bao hilo, Berkane waliongeza kasi ya mashambulizi wakitafuta kusawazisha lakini walikutana na upinzani mkali kutoka kwa safu ya ulinzi ya Al Hilal ambayo ilisimama imara kwa muda mrefu wa mchezo.

Hata hivyo, juhudi za wenyeji zililipa katika dakika za mwisho za mchezo baada ya Berkane kupata penati katika dakika za nyongeza, ambapo mshambuliaji Youssef Mehri alifunga bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1–1.

Bao hilo la dakika za mwisho limeifanya mechi ya marudiano kuwa wazi kwa timu zote mbili zitakapokutana tena Rwanda wiki ijayo kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya nusu fainali

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mshindi wa jumla kati ya RS Berkane na Al Hilal atakutana na mshindi wa mchezo kati ya AS FAR Rabat na Pyramids FC katika hatua ya nusu fainali.Β 

Hatua ya robo fainali ya CAF Champions League inaendelea leo kwa mchezo mwingine mkubwa utakaowakutanisha Esperance Sportive de Tunis ya Tunisia dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa mashindano hayo, Al Ahly ya Misri.Β 

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
49m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’