Mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England zimechukua sura mpya baada ya matokeo ya michezo iliyochezwa Jumamosi, Machi 14, 2026, ambapo vinara Arsenal walipata ushindi muhimu huku wapinzani wao wakubwa Manchester City wakiteleza na kupoteza pointi muhimu.
Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Emirates, Arsenal waliifunga Everton mabao 2β0 na kuimarisha uongozi wao kileleni mwa msimamo wa ligi. Ushindi huo uliwafanya kufikisha pointi 70, wakizidi Manchester City kwa tofauti ya pointi tisa ingawa City wana mchezo mmoja mkononi.
Arsenal walipata bao la kwanza dakika ya 89 kupitia mshambuliaji Viktor GyΓΆkeres, aliyefunga baada ya presha kubwa dhidi ya safu ya ulinzi ya Everton. Bao la pili lilifungwa katika dakika za majeruhi na kinda mwenye umri wa miaka 16, Max Dowman, aliyefunga kwa shambulizi la kushtukiza na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika historia ya Premier League.Β
Ushindi huo umeongeza matumaini ya Arsenal kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa ligi baada ya miaka 22 tangu walipofanya hivyo mwaka 2004.
Wakati huo huo, Manchester City waliteleza baada ya kutoka sare ya 1β1 dhidi ya West Ham United katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa London Stadium.
City walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kiungo Bernardo Silva katika dakika ya 31, lakini West Ham walisawazisha dakika chache baadaye kupitia beki Konstantinos Mavropanos, aliyefunga kwa kichwa baada ya kona kupigwa na Jarrod Bowen.Β
Licha ya City kumiliki mpira kwa muda mwingi na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga, walishindwa kupata bao la ushindi, matokeo yaliyopunguza kasi ya mbio zao za kuwania ubingwa.
Katika michezo mingine iliyochezwa siku hiyo, Newcastle United waliifunga Chelsea bao 1β0 kupitia Anthony Gordon, wakati Brighton walishinda 1β0 dhidi ya Sunderland kwa bao la Yankuba Minteh. Burnley na Bournemouth walitoka sare ya 0β0.Β
Kwa matokeo hayo, presha sasa inaongezeka kwa Manchester City katika mbio za ubingwa huku Arsenal wakiendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa tofauti ya pointi 9 wakifika alama 70 huku City wakiwa na alama 61 na mchezo mmoja mkononi.Β