International,Normal News,Arsenal, Manchester City, Everton, West Ham, Local

Arsenal wapanua uongozi Ligi Kuu England, Man City wateleza

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Mar 2026
Arsenal wapanua uongozi Ligi Kuu England, Man City wateleza

Mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England zimechukua sura mpya baada ya matokeo ya michezo iliyochezwa Jumamosi, Machi 14, 2026, ambapo vinara Arsenal walipata ushindi muhimu huku wapinzani wao wakubwa Manchester City wakiteleza na kupoteza pointi muhimu.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Emirates, Arsenal waliifunga Everton mabao 2–0 na kuimarisha uongozi wao kileleni mwa msimamo wa ligi. Ushindi huo uliwafanya kufikisha pointi 70, wakizidi Manchester City kwa tofauti ya pointi tisa ingawa City wana mchezo mmoja mkononi.

Arsenal walipata bao la kwanza dakika ya 89 kupitia mshambuliaji Viktor GyΓΆkeres, aliyefunga baada ya presha kubwa dhidi ya safu ya ulinzi ya Everton. Bao la pili lilifungwa katika dakika za majeruhi na kinda mwenye umri wa miaka 16, Max Dowman, aliyefunga kwa shambulizi la kushtukiza na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika historia ya Premier League.Β 

Ushindi huo umeongeza matumaini ya Arsenal kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa ligi baada ya miaka 22 tangu walipofanya hivyo mwaka 2004.

Wakati huo huo, Manchester City waliteleza baada ya kutoka sare ya 1–1 dhidi ya West Ham United katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa London Stadium.

City walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kiungo Bernardo Silva katika dakika ya 31, lakini West Ham walisawazisha dakika chache baadaye kupitia beki Konstantinos Mavropanos, aliyefunga kwa kichwa baada ya kona kupigwa na Jarrod Bowen.Β 

Licha ya City kumiliki mpira kwa muda mwingi na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga, walishindwa kupata bao la ushindi, matokeo yaliyopunguza kasi ya mbio zao za kuwania ubingwa.

Katika michezo mingine iliyochezwa siku hiyo, Newcastle United waliifunga Chelsea bao 1–0 kupitia Anthony Gordon, wakati Brighton walishinda 1–0 dhidi ya Sunderland kwa bao la Yankuba Minteh. Burnley na Bournemouth walitoka sare ya 0–0.Β 

Kwa matokeo hayo, presha sasa inaongezeka kwa Manchester City katika mbio za ubingwa huku Arsenal wakiendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa tofauti ya pointi 9 wakifika alama 70 huku City wakiwa na alama 61 na mchezo mmoja mkononi.Β 

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
49m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’