Mbeya City wapigwa 4G na Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Mar 2026
Mbeya City wapigwa 4G na Singida BS

Timu ya Singida Black Stars F.C. imepata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Mbeya City F.C.< katika mchezo wa NBC Premier League uliochezwa Jumapili, Machi 15, 2026, majira ya saa 10 jioni katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Stadium uliopo Babati, mkoani Manyara.

Katika mchezo huo wa ligi kuu Tanzania Bara, Singida Black Stars walionyesha kiwango kizuri hasa katika kipindi cha pili na kufanikiwa kuondoka na pointi tatu muhimu.

Mchezo ulianza kwa kasi huku Mbeya City wakionyesha nia ya kusaka ushindi mapema. Dakika ya 14, mshambuliaji Vitalis Mayanga aliifungia Mbeya City bao la kuongoza na kuwapa matumaini mashabiki wao.

Hata hivyo, furaha hiyo haikudumu kwa muda mrefu baada ya Singida Black Stars kusawazisha matokeo kupitia kwa Emmanuel Keyekeh aliyefunga kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 32 na kufanya matokeo kuwa 1-1 kabla ya mapumziko.

Kipindi cha pili kilishuhudia Singida Black Stars wakiongeza kasi ya mashambulizi na kuanza kutawala mchezo.

Dakika ya 70, Mossi Nduwumwe aliifungia Singida bao la pili na kuifanya timu yake kuanza kuongoza mchezo. Dakika nne baadaye, kiungo Ibrahim Imoro alifunga bao la tatu na kuongeza presha kwa Mbeya City.

Imoro alirudi tena kambani katika dakika ya 88, akifunga bao lake la pili binafsi na la nne kwa Singida Black Stars, bao lililohitimisha ushindi huo wa mabao 4-1.

Ushindi huo ni muhimu kwa Singida Black Stars katika mbio za kujipanga kwenye msimamo wa ligi, huku Mbeya City wakiendelea kutafuta matokeo bora katika mechi zao zijazo.Β 

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
19m ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
41m ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
1h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
2h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
2h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
5h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
7h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
8h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
8h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
10h ago
READ MORE β†’