Depu, Barker watwaa tuzo za ligi kuu February 2026

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th March 2026


Depu, Barker watwaa tuzo za ligi kuu February 2026

Mshambuliaji wa Yanga Laurindo Dilson 'Depu' amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya NBC kwa mwezi February 2026.

Depu ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Idd Suleiman 'Nado' wa Azam Fc na Rushine de Reuck wa Simba.

Mwezi February Depu aliifungia Yanga mabao mawili na kuwasaidia mabingwa hao watetezi ligi kuu ya NBC kushinda mechi mbili.

Aidha Mkufunzi wa Simba Steve Barker amechaguliwa kuwa kocha bora wa ligi kuu ya NBC kwa mwezi February 2026.

Barker ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Florent Ibenge wa Azam Fc na Pedro Goncalves wa Yanga ambao aliingia nao fainali.

Mwezi February, Barker aliiongoza Simba katika mechi tatu akishinda mbili na kutoka sare mechi moja na kuipandish Simba hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.