TAARIFA MPYA: Klabu ya Chelsea imeanzisha uchunguzi wa ndani kuhusu mshukiwa wa kuvujisha taarifa kutoka chumba cha wachezaji baada ya taarifa za kikosi kuvuja mara mbili ndani ya wiki moja kabla ya mechi kubwa dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG), ikiwa ni muda mfupi kabla ya mchezo wao wa pili.
Kwa sasa, CFC wako kwenye tahadhari kubwa wakitafuta chanzo cha uvujishaji huo wa mara kwa mara wa kikosi (Mailsport).
Chelsea itacheza mechi yake ya mkondo wa pili dhidi ya PSG usiku wa leo huku ikiwakosa wachezaji muhimu kama nahodha wao Reece james, Malo gusto, na wengineo.



