Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo kwa mechi za viporo ambapo mabingwa watetezi Yanga wako ugenini mkoani Arusha kuwakabili TRA United katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Ni katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka mkoani Arusha, hasa baada ya kutofanyika kwa mchezo kati ya TRA United dhidi ya Simba ambao ulipaswa kupigwa March 14 lakini mvua ikapelekea mchezo huo kuahirishwa.
Wenyeji TRA United watakuwa wakisaka alama tatu ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wakati Yanga inasaka ushindi ili kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi.
Mchezo mwingine utakaopigwa leo ni kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Singida BS utakaopigwa saa 2 usiku katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.




