Motsepe avunja ukimya sakata la Afcon 2025

Joel JJ By Joel JJ
•
19 Mar 2026
Motsepe avunja ukimya sakata la Afcon 2025

Rais wa CAF Patrice Motsepe, amevunja ukimya kufuatia uamuzi tata wa kuinyang’anya Senegal ubingwa wa Mataifa ya Afrika 2025 (AFCON) na kuipatia Morocco, akisisitiza kuwa maamuzi ya vyombo vya kisheria vya shirikisho hilo yanapaswa kuheshimiwa.

Motsepe alieleza kuwa uamuzi huo ulitolewa na kamati huru ya rufaa ya CAF kwa kuzingatia kanuni za mashindano, na hivyo haukuwa wa kisiasa bali wa kisheria. Amesisitiza kuwa CAF ina wajibu wa kusimamia sheria na kuhakikisha haki inatendeka kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Uamuzi huo ulitangazwa rasmi Machi 17, 2026, baada ya kamati ya rufaa kubaini kuwa timu ya Senegal ilikiuka kanuni kwa kuondoka uwanjani bila ruhusa ya mwamuzi wakati wa fainali dhidi ya Morocco. Kwa mujibu wa kanuni hizo, kitendo hicho kinachukuliwa kama kupoteza mechi, na hivyo matokeo kubadilishwa kuwa ushindi wa mabao 3-0 kwa Morocco.

Awali, Senegal walikuwa wameshinda mchezo huo kwa mabao 1-0 baada ya muda wa nyongeza, lakini mechi hiyo iligubikwa na utata mkubwa kufuatia wachezaji wao kutoka nje ya uwanja wakipinga penalti iliyotolewa kwa Morocco dakika za mwisho.

Hata hivyo, kauli ya Motsepe imekuja wakati kukiwa na upinzani mkubwa kutoka Senegal, ambapo serikali na shirikisho la soka la nchi hiyo zimeutaja uamuzi huo kuwa si wa haki na zimetangaza kupeleka rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Sakata hilo limeibua mjadala mpana barani Afrika na duniani, huku baadhi ya wadau wa soka wakikosoa uamuzi huo na wengine wakisisitiza umuhimu wa kufuata sheria za mchezo.

Licha ya presha hiyo, Motsepe amesisitiza kuwa CAF itaendelea kulinda misingi ya haki, uwazi na utawala bora katika soka la Afrika.

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
18m ago
READ MORE →
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE →
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE →
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE →
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE →
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE →
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE →
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE →
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE →
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE →