Local,Normal News,Simba, Azam, Pamba, Mashujaa

Simba yavutwa sharubu Mwanza, Azam Fc yakwama Kigoma

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Mar 2026
Simba yavutwa sharubu Mwanza, Azam Fc yakwama Kigoma

Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc wameshindwa kunufaika na matokeo ya watani zao Yanga baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba.

Jana Yanga ililazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya TRA United na kuibua shangwe kwa mashabiki wa Simba wakiamini wana nafasi ya kupunguza gap la pointi dhidi ya watani zao hao kwenye msimamo wa ligi.

Anicet Oura aliitanguliza Simba kwa bao safi kwenye dakika ya 33 lakini Pamba Jiji wakarejea mchezoni dakika tatu baadae James Mwashinga akifunga bao kwa shuti kali lililomshinda mlinda lango wa Simba Djibril Kassali kupitia mpira wa adhabu.

Licha ya kutawala mchezo huo, Simba walishindwa kuipenya ngome ya Pamba Jiji na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya sare.

Mchezo mwingine wa ligi kati ya Mashujaa Fc dhidi ya Azam Fc ulipigwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.

Matokeo hayo yamepelekea kutokuwa na mabadiliko makubwa kwenye msimamo wa ligi, Azam Fc wakiendelea kusalia nafasi ya pili huku Simba wakisogea nafasi ya tatu.

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
36m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
19h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’