Kamati ya saa 72 yafungia waamuzi walioshindwa kutafsiri sheria za soka

Joel JJ By Joel JJ β€’ 19th March 2026


Kamati ya saa 72 yafungia waamuzi walioshindwa kutafsiri sheria za soka

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), katika kikao chake cha March 17, 2026 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi na kufany maamuzi kama ifuatavy;

1. Singida BS FC 0-3 Young Africans SC (Mechi Na. 72)

  • Carlos Leonard Mayangura (Shabiki wa Yanga): Amefungiwa miezi 12 kwa kosa la kuongoza mashabiki kuvunja madirisha ya chumba cha kuvalia na kusababisha uharibifu.

  • Klabu ya Young Africans: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 na kutakiwa kulipa gharama za matengenezo ya madirisha na maeneo yaliyoharibiwa na mashabiki wao.

2. Singida BS FC 1-2 Simba SC (Mechi Na. 111)

  • Katanga Hussein (Mwamuzi): Amefungiwa mizunguko mitatu (3) kwa kushindwa kutafsiri sheria baada ya golikipa wa Simba, Djibrilla Kassali, kucheza rafu dhidi ya Joseph Guede (Singida BS) ndani ya eneo la penati.

  • Klabu ya Singida BS: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 kwa kosa la meneja wake, Othmen Najjar, kutovaa sare za timu kama maofisa wengine.

3. Azam FC 0-0 Young Africans SC (Mechi Na. 104)

  • Ally Mnyupe (Mwamuzi): Amefungiwa mizunguko mitatu (3) kwa kushindwa kutoa penati baada ya mchezaji wa Azam, Fuentes Mendoza, kucheza rafu dhidi ya Prince Dube (Yanga) ndani ya eneo la penati.

  • Klabu ya Azam FC: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 kwa kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia na badala yake kutumia njia ya kuingilia vyumbani (corridor).

  • Klabu ya Young Africans: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 kwa kosa la mashabiki wao kuwarushia chupa za maji waamuzi wakati wakitoka uwanjani baada ya mechi.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.