Local,Normal News,Yanga, Mtibwa

Kocha Yanga alia na ugumu wa Ratiba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Mar 2026
Kocha Yanga alia na ugumu wa Ratiba

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesisitiza kuwa kikosi chake hakipati muda wa kutosha wa maandalizi ya mechi kutokana na ratiba ngumu inayaowakabili.

Yanga iko mkoani Dodoma ambapo kesho Jumamosi, watashuka uwanja wa Jamhuri kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa mzunguuko wa 16 ambao ni wa kwanza duru ya pili.

Akizungumza na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Goncalves alisema kesho watacheza mechi ya 7 katika kipindi cha siku 21.

Amesema kwa takribani wiki tatu wanacheza ugenini katika mechi ambazo zinawalazimu kusafiri huku baadhi ya wachezaji wakiwa kwenye mfungo.

Hata hivyo kocha huyo raia wa Ureno amesisitiza kuwa pamoja na changamoto hizo, wataendelea kupambana wakijipanga kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

"Maandalizi yetu kuelekea mchezo wa kesho yamekuwa na changamoto kubwa. Tulitoka Arusha jana baada ya safari ndefu na tulipowasili hapa, wachezaji wengi walifanya mazoezi ya kurejesha nguvu (recovery), huku wengine wakifanya mazoezi mepesi uwanjani."

"Kwa kipindi cha wiki tatu hadi nne zilizopita tumekuwa na ratiba ngumu sana. Mchezo wa kesho utakuwa wa saba ndani ya siku 21 jambo ambalo ni changamoto kubwa. Pia tunapaswa kuzingatia kuwa baadhi ya wachezaji wako kwenye mfungo wa Ramadhani pamoja na safari za mara kwa mara kwa ujumla tunapitia kipindi kigumu sana cha msimu"

"Tumemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi tukiwa kileleni mwa msimamo. Hili halitupi ubingwa, lakini linatupa imani kubwa kuelekea siku zijazo. Sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar."

"Kwangu binafsi, huu ni mchezo wa kipekee. Ulikuwa mchezo wangu wa kwanza nikiwa na timu hii nyumbani uliochezwa KMC. Wakati huo hatukuwa kileleni tulikuwa nyuma kwa alama mbili dhidi ya wapinzani wetu. Sasa tupo juu ya msimamo tunapoanza mzunguko wa pili na kujiamini kutakuwa muhimu sana"

"Lengo letu siku zote ni pointi tatu na kesho haitakuwa tofauti. Pia ni muhimu kwetu kufika kwenye dirisha la mechi za kimataifa (FIFA) tukiwa kileleni bila kujali matokeo ya kesho. Kipindi hicho kitakuwa muhimu kwa mapumziko na kurejea kwa wachezaji, hasa kwa wale walio na majeraha na watakaojiunga na timu zao za taifa," alisema Goncalves

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’