Local,Normal News,Yanga, Mtibwa

Yanga yakwama Dodoma, sare ya tatu mfululizo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Mar 2026
Yanga yakwama Dodoma, sare ya tatu mfululizo

Bao la dakika za lala salama lililofungwa na Mtibwa Sugar kupitia mpira wa kona uliopigwa na Ismail Mhesa limewanyima Yanga alama tatu muhimu katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Wachezaji wa Yanga walimlalamikia mwamuzi kwa kuruhusu bao hilo licha ya mlinda lango Djigui Diarra kuonekana amesukumwa wakati akijaribu kuokoa mpira huo wa kona.

Yanga ilikuwa na kwanza kufunga bao la uongozi kupitia kwa Pacome Zouzoua kwenye kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya Emmanuel Mwanengo.

Hata hivyo wachezaji wa Yanga watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kuondoka na alama tatu katika mchezo huo kwani walitengeneza nafasi nyingi lakini changamoto ilikuwa katika kuweka mpira kimiani.

Ni sare ya tatu mfululizo Yanga inapata, pengine ni nyakati ngumu zaidi kutokea kwa Yanga kwenye ligi katika misimu ya karibuni.

Msimu uliopita Yanga ilipoteza mechi mbili mfululizo lakini wakati huu sare tatu mfululizo, Yanga ikianza kwa kuchechea mechi za duru ya pili.

Licha ya matokeo hayo, Yanga inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha alama 38, na kimahesabu wataendelea kuwa kileleni hata ikitokea timu nyingine zitashinda mechi zao za viporo.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
11h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
14h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
17h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
17h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
19h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
23h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’