Local,Normal News,Simba, TRA

Simba yaifumua TRA United 3-0, Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Mar 2026
Simba yaifumua TRA United 3-0, Ligi Kuu

Mnyama Simba Sc ametakata uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo leo akiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Unaweza kusema TRA United leo walikutana na soka la aina tofauti kabisa kutoka kwa vijana wa kocha Steve Barker waliokuwa na kiu ya alama tatu.

Simba iliandika bao la kwanza mapema tu kwenye dakika ya 12 kupitia kwa Suleiman Mwalimu aliyefunga bao lake la tano msimu huu.

Ulikuwa mkwaju wa penati baada ya Nickson Kibabage kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0, uongozi ambao uliwaongezea ari zaidi waliporejea kipindi cha pili.

Kasi ya Simba kupitia washambuliaji wa pembeni Libasse Gueye na Annicet Oura iliwapa wakati mgumu walinzi wa TRA United wakijikuta wanafanya madhambi mara kwa mara.

Kupitia mpira wa adhabu Neo Maema akaongeza bao la pili dakika ya 67 kabla ya Yusuph Kagoma kuongeza bao la tatu wakati mchezo ukielekea ukiongoni.

Ulikuwa mchezo ambao pengine Simba ingefunga mabao zaidi kama washambuliaji wake wangekuwa makini Elie Mpanzu akikosa miongoni mwa nafasi ya adimu dakika za lala salama.

Ni alama tatu muhimu kwa Simba ambazo zinawapaisha hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wakifikisha alama 31 na kuipiku Azam Fc yenye alama 29.

Simba bado ina mechi mbili za viporo dhidi ya vinara wa ligi hiyo Yanga wenye alama 38 baada ya mechi 16.

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’