CAF Champions League 2026 Quarter-"> CAF Champions League 2026 Quarter-">

Berkane, Mamelodi hizoo nusu fainali CAFCL

Joel JJ By Joel JJ • 22nd March 2026


Berkane, Mamelodi hizoo nusu fainali CAFCL

Hatua ya robo fainali ya CAF Champions League 2026 Quarter-finals imekamilika rasmi leo Jumapili baada ya kuchezwa kwa michezo ya mkondo wa pili iliyokuwa na ushindani mkubwa na matokeo ya kusisimua.

Katika mechi zilizochezwa leo, Mamelodi Sundowns walifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali licha ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Stade Malien ugenini. Sundowns walinufaika na ushindi wa mabao 3-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza, na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2.

Mchezo huo uliochezwa Bamako ulianza kwa kasi huku Stade Malien wakipata bao la mapema kabisa dakika ya kwanza na kuongeza lingine kabla ya mapumziko, lakini juhudi zao hazikutosha kuziba pengo la mabao ya mechi ya kwanza.

Katika mchezo mwingine, RS Berkane waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Al-Hilal Omdurman na kufuzu kwa jumla ya mabao 2-1. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika za mwisho, likiwaangusha wenyeji waliokuwa wakihitaji ushindi ili kusonga mbele.

Kwa matokeo hayo, RS Berkane wanaungana na Sundowns katika hatua ya nusu fainali, pamoja na FAR Rabat na Espérance de Tunis ambao walifuzu jana Jumamosi baada ya kuwashinda wapinzani wao katika michezo ya mkondo wa pili.

FAR Rabat waliitoa Pyramids kwa jumla ya mabao 3-2, huku Espérance de Tunis wakiiondosha Al Ahly kwa jumla ya mabao 4-2, matokeo yaliyoonyesha ushindani mkali katika hatua hiyo ya mashindano.

Kwa sasa, macho ya wadau wa soka barani Afrika yanaelekezwa katika hatua ya nusu fainali, ambapo timu hizo nne zinatarajiwa kuonesha kiwango cha juu zaidi katika harakati za kusaka ubingwa wa klabu bingwa Afrika.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.