Orlando City wamefikia makubaliano ya kumsajili Antoine Griezmann bila ada ya uhamisho kuanzia Julai 2026.
Timu hiyo ya MLS awali ilisisitiza kumsajili mwezi Machi, lakini Atlético Madrid walikataa ofa hiyo. Orlando waliendelea kuwa na dhamira, na sasa wamefanikiwa kufanikisha dili hilo, kila kitu kikiwa kimekubaliwa.
MARCA imeripoti, Griezmann anatarajiwa kusafiri kwenda Orlando wiki hii kukamilisha taratibu na kusaini mkataba wake. Nyota huyo wa Ufaransa atavaa jezi namba 7 na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na Orlando City.



