Rais wa Heshima wa klabu ya Simba Bilionea Mohamed Dewji 'Mo' amefanikisha mpango wa Wekundu hao wa Msimbazi kumuongeza mkataba winga Elie Mpanzu.
Mpanzu amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia wababe hao kutoka mitaa ya Msimbazi jijini Dar es salaam.
Kulikuwa na sintofahamu juu ya hatma ya Mcongomani huyo ndani ya Simba mengi yakizungumzwa wakati wa usajili wa dirisha dogo.
Hatimaye sasa ni rasmi, Mpanzu bado ni mali ya Simba kwa misimu mingine miwili.







