Mshambuliaji wa Liverpool, Alexander Isak, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki michezo ya robo fainali ya UEFA Champions league dhidi ya Paris Saint-Germany (PSG), baada ya kurejea katika hali nzuri ya kimwili.
Taarifa hizo zimethibitishwa na kocha mkuu wa Liverpool, Arne slot, ambaye amesema kuwa nyota huyo tayari amerejea mazoezini kwa kiwango kamili na anaendelea vizuri kuelekea kurejea uwanjani.
Isak alikuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na changamoto ya majeraha, hali iliyozua wasiwasi kwa mashabiki wa Liverpool kuelekea katika hatua muhimu ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya. Hata hivyo, kurejea kwake mazoezini kunatoa matumaini makubwa kwa timu hiyo kabla ya kuvaana na PSG katika hatua hiyo ya mtoano.
Kwa mujibu wa kocha Slot, mshambuliaji huyo anatarajiwa kurejea rasmi kikosini mara baada ya kumalizika kwa mapumziko ya kimataifa, hatua itakayoongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Liverpool wanapojiandaa kwa mechi hizo muhimu.
(Source: DaveOCKOP)