Kiungo mshambuliaji wa Simba Morice Abraham ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa na mashindano ya FIFA Series yatakayofanyika Rwanda katika kipindi hiki cha mapumziko ya kalenda ya FIFA.
Kocha Mkuu wa Stars Miguel Gamondi amethibitisha kuongezwa kwa Abraham ambaye amechukua nafasi ya Simon Msuva aliyeshindwa kujiunga na timu.





