Klabu ya RC Lens imekataa ombi la Paris Saint-Germain la kuahirisha mchezo wao muhimu wa kileleni mwa msimamo wa ligi.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka RMC Sport, PSG waliomba mechi hiyo isogezwe mbele kutokana na kubanwa na ratiba, ambapo mchezo huo unaangukia katikati ya michezo yao miwili ya UEFA Champions League dhidi ya Liverpool FC.
Hata hivyo, Lens ambao wanashika nafasi ya pili wakiwa nyuma kwa tofauti ya pointi moja tu, hawako tayari kutoa unafuu wowote kwa PSG katika kipindi hiki muhimu. Uamuzi huo unaifanya vita ya ubingwa wa ligi kuwa ngumu zaidi, huku PSG wakilazimika kupambana na ratiba ngumu ya ndani na kimataifa kwa wakati mmoja.



