Kamwe akiri Yanga imeyumba kwenye usajili

Joel JJ By Joel JJ β€’ 25th March 2026


Kamwe akiri Yanga imeyumba kwenye usajili

Unaweza kusema katika usajili wa madirisha mawili yaliyopita, Yanga haikufanya vyema kwa aina ya wachezaji waliowasajili.

Ukiangalia idadi kubwa ya wachezaji ambao walisajiliwa dirisha kubwa sasa hawapo huku wengine walioongezwa dirisha dogo wakishindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza.

Celestin Ecua, Moussa Balla Conte, Andy Boyeli na Mohamed Doumbia ni miongoni mwa nyota wa kigeni ambao walisajiliwa dirisha kubwa lakini wote wameondoka.

Kiungo mshambuliaji Allan Okello, Winga Buba Jammeh na mshambuliaji Laurindo Aurelio 'Depu' ni miongoni mwa wachezaji waliotua dirisha dogo lakini ni Okello na Depu pekee waliofanikiwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza Depu akiwa ameifungia Yanga mabao 11 katika mechi 10 kwenye mashindano yote.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amekiri kutofanya vyema katika madirisha hayo ya usajili huku akitaja sababu ni mabadiliko ya utaratibu wa usajili.

Kamwe amebainisha kuwa katika madirisha hayo jukumu la mapendekezo ya usajili yaliachwa kwa makocha.

"Tofauti na misimu mingine, msimu huu usajili umesimamiwa na makocha kwa 100%, viongozi walikuwa na jukumu la kutimiza tu mahitaji ya makocha hao."

"Usajili wa dirisha kubwa ulisimamiwa na kocha Romain Folz wakati kwenye dirisha dogo, usajili ulisimamiwa na kocha wetu, Pedro Goncalves kwa asilimia 100%."

"Nafikiri hili ni eneo ambalo tunapaswa kulirekebisha na nitumie nafasi hii kumuomba Rais wa klabu Injini Hersi Said kwamba anahitajika sana kurudi kwenye hili zoezi yaani yeye mwenyewe asimamie usajili kama ilivyokuwa awali. Nafikiri haya mambo ya usajili yanapaswa kurudi kwenye himaya yake," alisema Kamwe


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.