International,Normal News,Local, Nottingham, Tottenham

Hawa Spurs Championship inawaita

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Mar 2026
Hawa Spurs Championship inawaita

Klabu ya Tottenham Hotspur imeingia katika hofu kubwa ya kushuka daraja kufuatia kipigo kizito cha mabao 3-0 kutoka kwa Nottingham Forest mwishoni mwa wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Katika pambano hilo muhimu kwa pande zote mbili zilizokuwa zikisaka pointi za kujinasua kutoka mkiani, Forest walionyesha ubora mkubwa kwa kufunga mabao kupitia Morgan Gibbs-White,Taiwo Awoniyi pamoja na Igor Jesus, na kuondoka na ushindi mnono uliowaacha Spurs hoi.

Matokeo hayo yameifanya Tottenham kushuka hadi nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi, wakibaki juu ya mstari wa kushuka daraja kwa tofauti alama moj tu dhidi ya West Ham. Spurs wana alama 30 huku West Ham wakiwa na alama 29. Hali hiyo imezidisha presha kwa kikosi hicho ambacho kimekuwa kikisuasua kwa muda mrefu sasa.

Tottenham wanakabiliwa na rekodi mbaya ya kutopata ushindi katika mechi kadhaa mfululizo za ligi, jambo linaloonyesha wazi kuporomoka kwa kiwango cha timu hiyo. Ulinzi wao umekuwa dhaifu, huku safu ya ushambuliaji ikishindwa kutumia nafasi wanazozipata.

Kwa upande mwingine, ushindi huo umeipa Nottingham Forest nguvu mpya katika harakati zao za kubaki ligi kuu, wakipanda juu ya Tottenham katika msimamo baada ya kufikisha alama 32.

Kocha wa Tottenham, Igor Tudor, sasa anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki na uongozi wa klabu hiyo, huku wengi wakitaka mabadiliko ya haraka ili kuinusuru timu isishuke daraja.

Mashabiki wa Spurs walionyesha kutoridhishwa kwao wakati wa mchezo huo, baadhi wakiondoka uwanjani kabla ya kipenga cha mwisho, ishara ya kuchoshwa na matokeo mabaya yanayoendelea.

Huku msimu ukiwa unaelekea ukingoni, Tottenham sasa wanakabiliwa na mechi chache zilizosalia ambazo zinaweza kuamua hatima yao. Wataalamu wa soka wanaamini kuwa bila mabadiliko ya haraka ya mbinu na morali ya wachezaji, klabu hiyo inaweza kujikuta ikishuka daraja kwa mara ya kwanza katika kipindi kirefu.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’