SIMBA SC KUREJEA MAZOEZINI KUJIANDAA DHIDI YA COASTAL NA AZAM

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 26th March 2026


SIMBA SC KUREJEA MAZOEZINI KUJIANDAA DHIDI YA COASTAL NA AZAM

Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kurejea rasmi mazoezini kesho, Ijumaa Machi 27, 2026, kuanza maandalizi ya michezo miwili muhimu ya mashindano ya ndani.

Kwa mujibu wa ratiba, Simba SC itaanza kwa kuikaribisha Coastal Union mnamo Aprili 2, kabla ya mchezo wao wa dabi dhidi ya Azam FC utakaochezwa Aprili 5.

Mechi hizo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku Simba SC ikilenga kupata matokeo chanya ili kuimarisha nafasi yake katika msimamo wa ligi.

Maandalizi hayo yanaanza mapema ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha kikosi kinakuwa katika kiwango bora kuelekea michezo hiyo muhimu.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.