Local,Normal News,Yanga

Takwimu bado zinambeba Goncalves Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Mar 2026
Takwimu bado zinambeba Goncalves Yanga

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Pedro Goncalves, unaweza kusema kwa kuangalia takwimu 'hajafeli' lakini kinachofanya ahukumiwe ni pale timu yake inaposhindanishwa na Yanga ya msimu uliopita.

Pedro alitambulishwa rasmi Oktoba 25, 2025 siku ambayo Yanga SC ilikuwa dimbani ikicheza dhidi ya Silver Strikers katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku yeye akifuatilia mchezo huo kwa njia ya televisheni.

Kocha huyo alianza rasmi majukumu yake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu, ushindi ulioweka msingi wa mwenendo mzuri kwenye ligi.

Katika kipindi chake hadi sasa, Pedro ameiongoza Yanga katika jumla ya michezo 26 kwenye michuano minne tofauti ambayo ni Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho la CRDB na Kombe la Mapinduzi.

Kwa mujibu wa takwimu, kati ya michezo hiyo 26:

  • Amefanikiwa kushinda michezo 17
  • Sare 7
  • Kupoteza mara 2 pekee

Aidha, timu imefunga jumla ya mabao 48 huku ikiruhusu mabao 8 tu, ikiashiria uimara mkubwa wa safu ya ulinzi pamoja na ufanisi wa ushambuliaji.

Katika Ligi Kuu pekee, Pedro ameiongoza Yanga kushinda michezo 10 kati ya 14 na kutoka sare mechi 4. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, timu imeshinda mechi 2, sare 2 na kupoteza 2.

Kwa upande wa Kombe la Mapinduzi, Yanga iliibuka mabingwa ikishinda mechi 3 na kutoka sare 1, huku kwenye Kombe la Shirikisho la CRDB ikishinda michezo yote miwili iliyocheza.

Sare tatu mfululizo katika mechi za ligi kuu ndio matokeo yaliyoweka rehani kibarua chake kabla ya uongozi wa Yanga kuridhia aendelee na majukumu yake baada ya tathmini huku wakimuongezea nguvu kwa kumrejesha Kocha Msaidizi Abduhamid Moalin.

Bado kikosi chake kiko kileleni mwa msimamo wa ligi huku akiahidia kurejesha ubingwa wa ligi Jangwani kwa msimu wa tano mfululizo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’