Stars yajipanga kuikabili Macau FIFA Series Rwanda

Joel JJ By Joel JJ β€’ 27th March 2026


Stars yajipanga kuikabili Macau FIFA Series Rwanda

Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Liechtenstein jana, kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimerjea mazoezini nchini Rwanda kujiandaa na mchezo wa pili dhidi ya Macau utakaopigwa Jumapili, March 29 dimba la Kigali, Pele huko Rwanda.

Vijana wa kocha Miguel Gamondi wanahitaji kushinda mchezo huo ili kumaliza machungu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya vibonde Liechtenstein.

Macau walipigwa mabao 4-1 na Aruba katika mchezo wao uliopita. Ni kama mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kwani timu zote zilipoteza mechi zao za kwanza huku Aruba na Liechtenstein zikitarajiwa kuchuana kwenye mchezo wa fainali.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.