Local,Normal News,Yanga

Yanga yafunguka kumkosa Diarra

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Mar 2026
Yanga yafunguka kumkosa Diarra

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe anasema kufungiwa kwa golikipa wao, Djigui Diarra hakutawaathiri kwa kuwa wapo magolikipa wengine wawili wenye ubora.

Juzi Diarra alikumbana na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi (Kamati ya saa 72) kufuatia matukio ya utovu wa nidhamu aliyofanya kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Pamoja na kufungiwa mechi tatu, Diarra pia alitakiwa kulipa faini ya jumla ya Tsh Milioni 4.

Kamwe amesema Yanga ina walinda lango wengine bora Aboutwalib Mshery 'Djigui Mshery' na Hussein Masalanga ambao wako tayari kuliweka salama lango la mabingwa hao watetezi.

"Tumepata taarifa ya kufungiwa mechi tatu golikipa wetu namba moja Djigui Diarra lakini niwahakikishie mashabiki na wanachama wetu, tunao magolikipa wengine bora ambao wataliweka salama lango la Yanga"

"Tunaye Aboutwalib Mshery ambaye kila anapopata nafasi pale Diarra anapokosekana yeye huondoka na cleen-sheet. Amefanya hivyo kwenye ligi na hata katika michuano ya kombe la Mapinduzi."

"Lakini pia tunaye Hussein Masalanga maarufu 'kipa la Afcon' ambaye nae yuko tayari kama benchi la ufundi litampa jukumu la kukaa langoni wakati ambao Diarra anakosekana," alisema Kamwe.

Kamwe amesema Yanga inatarajiwa kuingia kambini siku ya Jumatatu, March 30 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa April 04 uwanja wa KMC Complex.

Akizungumzia hali za majeruhi, Kamwe amesema wachezaji Prince Dube, Ibrahim Bacca, Edmund John na Chadrack Boka wameanza mazoezi mepesi huku mshambuliaji Depu akiendelea kusalia kwenye uangalizi wa daktari.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’