Local,Normal News,Yanga, Simba

Simba yamkomalia Damaro, shauri la uraia lasogezwa mbele TFF

Joel JJ By Joel JJ
28 Mar 2026
Simba yamkomalia Damaro, shauri la uraia lasogezwa mbele TFF

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeahirisha hadi wiki ijayo shauri lililofunguliwa na Simba SC dhidi ya mchezaji wa Yanga Mohamed Damaro Camara kuhusiana na uraia wa kiungo huyo.

Imeelezwa sababu ya kuahirishwa ni kuchelewa kwa Yanga na mchezaji Damaro kupokea wito rasmi wa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Hadhi na Sheria za Wachezaji za TFF.

Simba imefungua shauri hili ikidai kuwa Yanga wamekiuka kanuni za ligi kwa kuwa na wachezaji 13 wa kigeni, huku kanuni zikiruhusu wachezaji 12 tu.

Mohamed Damaro Camara anacheza kama mchezaji wa Tanzania, jambo ambalo Simba wanasema ni kinyume na taratibu za FIFA kuhusu kubadili uraia wa mchezaji (switching of nationality).

Kwa mujibu wa Simba, hatua hiyo ya Damaro kucheza kama Mtanzania bila kufuata mchakato rasmi wa FIFA inakiuka kanuni za mashindano.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE →
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE →
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE →
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE →
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE →
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE →
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE →