Local,Normal News,Azam, Singida

Singida BS yaipania Azam Fc April 1

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Mar 2026
Singida BS yaipania Azam Fc April 1

Jumatano April 1 2026 Singida Black Stars wataikaribisha Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa uwanja wa Airtel, mkoani Singida.

Baada ya kupoteza mechi mbili kubwa dhidi ya Yanga (3-0) na Simba (2-1) katika uwanja wake wa nyumbani, Singida BS inahitaji kujisahihisha dhidi ya 'mkubwa' mwingine kutoka jijini Dar es salaam.

Ukiacha mechi hizo walizopoteza dhidi ya 'wakubwa' hao kutoka Kariakoo, Singida BS imekuwa na mwenendo mzuri katika mechi zilizopita ikiibuka na ushindi.

Katika mechi tano zilizopita, Singida BS wamepoteza mechi mbili pekee dhidi ya Yanga na Simba na kushinda tatu.

Kwenye msimamo wa ligi wanashika nafasi ya sita wakiwa na alama 25 ambapo ushindi dhidi ya Azam Fc unaweza kuwasogeza hadi nafasi ya nne.

Kwa upande wa Azam Fc inayonolewa na kocha Florent Ibenge, ni timu ngumu kufungika msimu huu licha ya kuwa imedondosha alama nyingi kupitia matokeo ya sare.

Azam Fc haijapoteza mchezo wowote katika mechi 15 walizocheza duru ya kwanza. Lakini katika mechi tano zilizopita, imeshinda mechi moja tu na kutoka sare nyingine nne. Inashikilia nafasi ya tatu ikiwa imekusanya alama 29 baada ya kushuka dimbani mara 15.Β 

Mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex, ulimalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana.

Je Singida BS wataweza kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani siku ya Jumatano?

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’