Kenya yakamilisha malipo kuandaa Afcon 2027

Joel JJ By Joel JJ • 31st March 2026


Kenya yakamilisha malipo kuandaa Afcon 2027

Katika hatua kubwa kwa sekta ya michezo Afrika Mashariki, serikali ya Kenya imekamilisha malipo ya ada ya kuandaa Africa Cup of Nations (AFCON) 2027 kwa kuwasilisha kiasi cha KSh 3.9 bilioni (USD 30 milioni) kwa Confederation of African Football (CAF).

Hii inakuja baada ya msukumo mkubwa na hatari ya kupoteza nafasi ya kuwa miongoni mwa wenyeji wa fainali za mashindano y Afcon 2027 kwa ushirikiano wa nchi za Tanzania na Uganda.

Waziri wa Michezo wa Kenya, Salim Mvurya, alithibitisha Jumatano, Machi 31, 2026, kwamba serikali imekamilisha malipo hayo kabla ya muda wa mwisho tarehe 30 Machi, akisema hatua hiyo inaonyesha dhamira ya nchi kuhakikisha kuwa AFCON 2027 inafanyika kwa mafanikio ndani ya mipaka ya Kenya.

“Kwa kutimiza wajibu wetu, Serikali ya Kenya imewasilisha ada ya kuandaa AFCON kwa CAF, tukithibitisha uaminifu wetu, uwezo na dhamira thabiti ya kutoa mashindano ya hadhi ya juu,” alisema Mvurya katika taarifa yake.

Malipo haya ya ada ni sehemu ya makubaliano ya pamoja ya “Pamoja AFCON 2027”, ambapo Kenya, Uganda na Tanzania wanashirikiana kuandaa mashindano hayo kubwa yanayotazamiwa kufanyika kati ya 19 Juni hadi 18 Julai 2027, hatua ambayo itakuwa ya kihistoria kwa Afrika Mashariki.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.