Mashabiki wa Yanga SC wanapumua kwa faraja baada ya Laurindo Aurelio 'Depu', mshambuliaji hatari kutoka Angola, kuanza mazoezi na kikosi chake.
Hii habari njema kwa Wananchi kwani wanarejesha nguvu zao kuelekea mizunguko ya ligi inayofuata na mapambano ya kutetea ubingwa.
Depu alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya misuli, jambo lililosababisha hofu kidogo miongoni mwa mashabiki kwamba angekaa nje kwa muda mrefu.
Lakini kwa kuonyesha uthabiti na juhudi, mshambuliaji huyu amepambana kuhakikisha anarejea mapema, akiwa tayari kupambana kwenye mechi zijazo.
Akiwa amesajiliwa Yanga katika dirisha dogo la usajili, Depu anaonekana kuwa kinara wa mabao. Katika mechi 10 za mashindano mbalimbali, amefunga mabao 11, ikiwa ni takwimu ya kutisha kwa wapinzani. Kwenye ligi ya NBC, yuko sawa na mshambuliaji mwenzake Prince Dube, kila mmoja akiwa na mabao 6.
Pia ni furaha kubwa kwa Yanga kwamba wachezaji wengine waliokuwa majeruhi tayari wamerejea kikosini, wakiwemo beki tegemeo Ibrahim Hamad Bacca, pamoja na Chadrack Boka na Edmun John.Β
Kikosi cha Yanga kilirejea mazoezini jana kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumamosi, April 04 uwanja wa KMC Complex.




