Makocha Singida BS, Azam Fc watambiana

Joel JJ By Joel JJ β€’ 31st March 2026


Makocha Singida BS, Azam Fc watambiana

Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, Othmen Najjar, amesema kikosi chake kimekamilisha maandalizi kwa umakini mkubwa kuelekea mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Jumatano April 1 katika uwanja wa Airtel huko Singida.

Najjar ameeleza kuwa wamejikita zaidi katika kuimarisha mbinu za ushambuliaji na ulinzi, huku akiwataka wachezaji wake kucheza kwa nidhamu, umakini na kujiamini ili kupata matokeo chanya.

Kwa upande wake, winga wa Singida Black Stars, Ayoub Lyanga, amesema lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanaitumia vyema faida ya kucheza nyumbani kwa kupata ushindi.

Nae mkufunzi wa Azam Fc Florent Ibange amesema wanajua wanakwenda kukabiliwa na mechi ngumu mbele ya Singida BS watakaokuwa kwenye uwanja wa nyumbani.

Hata hivyo Ibenge amesema amekiandaa kikosi chake kikamilifu kuweza kuibuka na ushindi.

"Haitakuwa mechi nyepesi, Singida BS sio timu ndogo, msimu uliopita sisi (Azam Fc) tulimaliza nafasi ya tatu na Singida ya nne. Sote tumecheza kombe la Shirikisho (CAFCC) na kufika hatua ya makundi. Hivyo kesho itakuwa mechi kubwa inayozikutanisha timu ambazo ziliiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya CAF"

"Najua hatujawa na mfululizo wa matokeo mazuri mbele ya Singida BS hapa lakini niseme tumekuja kubadili historia hiyo, tuko hapa kwa ajili ya kushinda," alisema Ibenge

Beki wa Azam Fc, Nathaniel Chilambo amesema kwa maandalizi waliyonayo hawahitaji kupoteza mchezo huo wala kupata sare na badala yake ni kupata ushindi.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.