International,Transfer News,Local, Tottenham, Marseille

De Zerbi akubali kutua Spurs, asaini miaka mitano

Joel JJ By Joel JJ
β€’
31 Mar 2026
De Zerbi akubali kutua Spurs, asaini miaka mitano

Klabu ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kumshawishi kocha Muitaliano, Roberto De Zerbi, amekubali kujiunga na timu hiyo kwa mkataba wa muda mrefu wa miaka mitano.

De Zerbi ambaye kwa sasa hana timu tangu alipoondoka Marseille mapema mwaka huu, anachukua mikoba ya kuinoa Spurs, klabu inayopitia kipindi kigumu kwenye Ligi Kuu England.

Hatua ya Spurs kumuajiri kocha huyo imekuja kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa muda Igor Tudor, aliyeachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote baada ya kuhudumu kwa kipindi kifupi.Β 

De Zerbi ameripotiwa kukubali dili hilo na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano utakaodumu hadi mwaka 2031.Β 

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 anatambulika kwa mtindo wake wa soka la kushambulia na kumiliki mpira, aliouonyesha alipokuwa akiinoa Brighton, ambapo aliisaidia timu hiyo kufuzu michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Kwa upande wa Spurs, kipaumbele kikubwa kwa sasa ni kuhakikisha wanabaki ndani ya Ligi Kuu, huku ujio wa De Zerbi ukionekana kama suluhisho la haraka na la muda mrefu kwa changamoto zinazowakabili.

De Zerbi anatarajiwa kuanza kazi mara moja akipewa jukumu la kuinusuru timu hiyo pamoja na kuijenga upya kwa ajili ya ushindani wa misimu ijayo.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’