Baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili kupisha kalenda ya FIFA, mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea wiki hii ambapo leo mchezo mmoja utapigwa.
Singida BS itakuwa mwenyeji wa Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Airtel mkoani Singida.
Ni mechi inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali ikizikutanisha timu mbili ambazo msimu huu zilikuwa wawakilishi wa nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la CAF (CAFCC).
Ni vita ya mapema kuwania nafasi nne za juu kwenye msimamo kwa sasa Singida BS wakiwa nafasi ya 6 na alama 25 wakati Azam Fc wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 29.
Mchezo mwingine unatarajiwa kupigwa kesho Alhamisi, April 02 Simba ikiikaribisha Coastal Union mchezo utakaopigwa uwanja wa Isamuhyo.
Hii hapa ratiba ya mechi zote wiki hii;

