Local,Normal News,Simba, Coastal

Matola apania alama tatu dhidi ya Coastal Union, Muya aahidi kuwazuia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Apr 2026
Matola apania alama tatu dhidi ya Coastal Union, Muya aahidi kuwazuia

Kocha Msaidizi wa Simba Suleiman Matola amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union yamekamilika na wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Matola alisema wanatambua ugumu wa mchezo ulio mbele yao hasa kutokana na ubora wa wapinzani wao ambao mara nyingi wamewapa changamoto kila walipokutana.

Matola amesema wamewafuatilia wapinzani wao na kubaini ubora na udhaifu wao ambao watakwenda kuutumia siku ya kesho katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Isamuhyo.

"Mechi dhidi ya Coastal Union huwa inakuwa ngumu, katika kuthibitisha hilo mchezo w mzunguuko wa kwanza msimu uliopita uliisha kwa sare"

"Ila tumeangalia mazuri na mapungufu yao ili kuwazidi na kuibuka na ushindi hapo kesho"

"Lengo letu ni kuwa bora dhidi yao katika mchezo huo na hatimaye kuweza kuondoka na alama zote tatu," alisema Matola

Nae Kocha Mkuu wa Coastal Union Mohamed Omary Muya amesema amekiandaa kikosi chake kukabiliana na Simba huku wakilenga kushinda mchezo huo.

Muya amesema anatambua ubora wa klabu ya Simba hivyo wanahitaji kucheza kwa tahadhari huku wakiongeza ufanisi kwenye matumizi ya nafasi

"Tunatambua uwezo wa Simba lakini tumekuja kupambana kutafuta Alama Tatu muhimu. Wachezaji wetu wako vizuri kwenye utimamu wa Mwili kuelekea Mchezo wa Kesho"

"Tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi kwenye mechi zetu lakini hatuzitumii vyema, tumefanya kazi kubwa kwenye uwanja wa mazoezi ili kuhakikisha kesho tunaweza kutumia vyema nafasi. Kama wachezaji wetu wakifuata maelekezo vizuri natumai mashabiki wa Coastal Union watafuraho kesho, " alisema Muya

Simba na Coastal Union zitachuana kesho Alhamisi, April 02 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es salaam

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’