Local,Normal News,Yanga, Prisons

Pacome Zouzoua Atoa Ujumbe wa Kishujaa kwa Mashabiki wa Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Apr 2026
Pacome Zouzoua Atoa Ujumbe wa Kishujaa kwa Mashabiki wa Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua, amewapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kufuatia matokeo yasiyoridhisha ya hivi karibuni kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Pacome ameweka wazi kuwa wachezaji wa timu hiyo wanatambua deni kubwa walilonalo kwa mashabiki wao, na wamejipanga kuhakikisha wanarejea kwenye ubora wao haraka iwezekanavyo.

Akizungumza kwa kujiamini, Pacome alikiri kuwa msimu huu umekuwa na changamoto, lakini akaweka bayana kuwa bado kuna nafasi ya kurekebisha mambo:

"Msimu huu umekuwa mgumu kidogo lakini bado haujaisha. Haya ni mambo ya kawaida kwenye mpira na hata kwenye maisha ya kawaida ziko nyakati za kupita vipindi vigumu."

Nyota huyo alieleza kuwa kikosi kizima cha Yanga kimeanza mazoezi kwa ari mpya, kikilenga kurejesha kiwango chao bora:

"Jambo muhimu ni kukubali hali hii na kuongeza bidii uwanja wa mazoezi ili kuhakikisha tunarejea tukiwa imara zaidi."

"Tumerejea mazoezini tukiwa na umakini mkubwa, tutafanya mazoezi kwa bidii ili turejee kwenye ubora wetu na kuwapa furaha mashabiki," alisema

YangaΒ sasa wanajiandaa kwa mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa katika dimba la KMC Complex siku ya Jumamosi.

Mchezo huo utakuwa kipimo kwa mabingwa hao watetezi kuona kama wako tayari kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo baada ya sare tatu mfululizo kabla ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Katika mpango wa kuboresha zaidi, Yanga ilimrejesha aliyekuwa Mkurugenzi wa ufundi Abdulhamid Moalin wakimkaidhi majukumu ya kocha msaidizi ili kumsaidia Pedro Goncalves alikiri kuwa na wakati mgumu hasa kwenye mechi za ugenini.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’