Klabu ya FC Barcelona inaongoza mbio za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Bernardo Silva bure katika dirisha la majira ya kiangazi.
Iwapo dili hilo litakamilika, linaweza kuashiria mwisho wa enzi kwa nyota huyo ndani ya Manchester City baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa kwa kipindi cha miaka tisa.
Katika muda wake ndani ya City, Silva amefanikiwa kutwaa mataji mbalimbali makubwa yakiwemo:
- Premier League mara kadhaa
- UEFA Champions League mara 1
- FA Cup
- Kombe la Ligi (League Cup)
- UEFA Super Cup
- Kombe la Dunia la Klabu (FIFA Club World Cup)
- Community Shield
Barcelona wanaona usajili wa Silva kama fursa muhimu ya kuongeza uzoefu na ubora ndani ya kikosi chao, huku wakitarajia kumleta bila gharama ya uhamisho.
(Taarifa: Sun Sport)



