Gennaro Gattuso hatakuwa kocha wa Italy national team, huku mpango huo ukitajwa kufikia tamati rasmi.
Maamuzi hayo yanakuja kufuatia presha kubwa ndani ya timu ya taifa baada ya Italia kushindwa kufuzu kushiriki FIFA World Cup 2026, kufuatia kipigo cha kushangaza dhidi ya Bosnia and Herzegovina national team katika hatua ya mtoano.
Matokeo hayo yameibua mjadala mkubwa na kupelekea mabadiliko ya haraka katika benchi la ufundi, huku mashabiki na wachambuzi wakitaka mwelekeo mpya wa timu hiyo.
Kwa sasa, Antonio Conte na Massimiliano Allegri ndio majina yanayoongoza kupewa jukumu la kuinoa Italia, huku uongozi ukitarajiwa kufanya uamuzi wa mwisho hivi karibuni.