Local,Normal News,Yanga

Dube aongeza mzuka Yanga ikirudi Avic Town

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Apr 2026
Dube aongeza mzuka Yanga ikirudi Avic Town

Klabu ya Yanga imepata faraja baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Prince Dube kurejea rasmi kikosini kufuatia kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua kwa kipindi cha hivi karibuni.

Dube amerejea leo akianza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Jumamosi, Aprili 4, 2026 katika Uwanja wa KMC Complex.

Urejeo wa Dube ni habari njema kwa benchi la ufundi la Yanga, hasa katika kipindi hiki ambacho timu inapambana kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi. Yanga iliwakosa washambuliaji wake wote tegemeo Dube na Depu katika mechi za mwisho kabla ya mapumziko ya kalenda ya FIFA kutokana na majeraha.

Mbali na Dube, Yanga pia imepokea habari njema ya kurejea kwa nyota wengine waliokuwa majeruhi ambao sasa wameanza mazoezi. Wachezaji hao ni pamoja na Depu, Chadrack Boka, Edmund John na Ibrahim Hamad maarufu kama 'Bacca'.

Yanga waingia kambini Avic Town

Katika hatua nyingine, kikosi cha Yanga kimeingia rasmi kambini Avic Town kukamilisha maandalizi ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons

Awali, timu hiyo ilikuwa ikifanya mazoezi yake katika Uwanja wa KMC Complex, wakati maboresho ya miundombinu yalipokuwa yakifanyika katika kambi ya Avic Town.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
7m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
36m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’